Kwenye podikasti ya leo, Professa David Monda anazungumza naye Rehema Majollo, mwanzilishi na mwendeshaji wa Habari Academy, ambacho ni kituo cha kutoa mafunzo ya Kiswahili Marekani kupitia kwa njia ya mtandao. Majollo anazungumzia sababu za kuanzisha kituo hicho, changamoto za kufundisha Kiswahili Marekani na masuala mengine yanayohusu jamii ya Waafrika Marekani. Karibu!